Vortex Stay
VORTEXSTAY

VORTEX COMPANY AGENT REGISTRATION

Tayari Umejisajili? Ingia kama Wakala

Kama tayari umesajiliwa na kuidhinishwa, ingia kwenye akaunti yako ya wakala. Kama bado hujathibitishwa, wasiliana na Vortex Stay au kamilisha usajili wako hapa chini.

— au jisajili kama mtoa huduma mpya hapa chini —

Masharti ya Mawakala na Sera ya Faragha

Soma kwa makini kabla ya kuendelea na usajili wako.
Please read carefully before continuing with your registration.

VORTEX STAY

MASHARTI YA MAWAKALA NA SERA YA FARAGHA

Tarehe ya Kuanza Kutumika: 06 Septemba 2026 · Toleo: 1.0

Hati hii inaeleza masharti, wajibu, vigezo vya usajili, matumizi ya kitambulisho cha wakala, mwenendo unaotarajiwa, pamoja na namna Vortex Stay inavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa binafsi za mawakala.

Kwa kujisajili kupitia mfumo wa Vortex Stay unaopatikana kupitia artificialintelligence.tz, kuwasilisha taarifa zako na kukubali masharti haya, unathibitisha kuwa umeyasoma, umeyaelewa na umekubali kuyafuata.

SEHEMU A — MASHARTI NA VIGEZO VYA KUWA WAKALA

1. Sifa za Msingi za Mwombaji

Ili mtu akubalike kuomba kuwa wakala wa Vortex Stay anatakiwa:

  • Awe na umri wa miaka 18 au zaidi.
  • Awe na namba halali ya simu inayoweza kuthibitishwa kwa OTP.
  • Atumie majina yake halisi.
  • Awasilishe picha yake halisi na ya sasa.
  • Awasilishe taarifa sahihi za eneo analoishi au kufanyia kazi, ikijumuisha Mkoa, Wilaya na Tarafa pale inapohitajika.
  • Asiwasilishe taarifa za mtu mwingine kwa lengo la kupata kitambulisho cha wakala.
  • Awe tayari kufuata masharti, taratibu, maelekezo na kanuni za Vortex Stay.
  • Awe tayari kuthibitisha taarifa zake pale Vortex Stay itakapohitaji uthibitisho wa ziada unaoruhusiwa kisheria.

Kujisajili pekee hakumaanishi kwamba mwombaji amekubaliwa kuwa wakala.

2. Usajili wa Wakala

Mwombaji atatakiwa kujaza taarifa zinazohitajika kwenye mfumo, ambazo zinaweza kujumuisha:

  • Majina kamili;
  • Namba ya simu;
  • Mkoa;
  • Wilaya;
  • Tarafa;
  • Picha ya pasipoti;
  • Taarifa nyingine zinazohitajika kwa ajili ya uthibitishaji wa wakala.
  • Wakala yoyote hataruhusiwa kusajili akaunti zaidi ya moja kwenye mfumo.
  • Usajili katika mfumo haukupi haki ya kudai kamisheni mpaka uthibitisho utolewe.

Namba ya simu inaweza kuthibitishwa kupitia OTP. Baada ya kukamilisha usajili, taarifa zitatumwa kwa Vortex Stay kwa ajili ya ukaguzi.

3. Kuidhinishwa kwa Wakala

Mtu hatakuwa wakala aliyeidhinishwa mpaka ombi lake litakapokubaliwa na Vortex Stay. Vortex Stay ina haki ya:

  • Kukubali ombi;
  • Kukataa ombi;
  • Kuomba taarifa zaidi;
  • Kurudisha ombi kwa marekebisho;
  • Kusimamisha uhakiki;
  • Kusitisha au kufuta hadhi ya wakala pale masharti yatakapokiukwa.

Uamuzi wa kuidhinisha wakala unaweza kuzingatia usahihi wa taarifa, mahitaji ya biashara, eneo la huduma, usalama wa mfumo, na vigezo vinavyoweza kubadilika kulingana na mahitaji ya biashara.

4. Kitambulisho cha Vortex Stay Agent

Baada ya kuidhinishwa, wakala anaweza kupewa Vortex ID/Agent ID ya kipekee pamoja na kitambulisho cha kidijitali au cha kawaida. Kitambulisho hicho:

  • Kitatumika kumtambua wakala;
  • Hakitakiwi kuhamishwa kwa mtu mwingine;
  • Hakitakiwi kuuzwa, kukodishwa au kukopeshwa;
  • Hakitakiwi kubadilishwa au kughushiwa;
  • Kinaweza kusimamishwa au kufutwa endapo wakala atakiuka masharti.

Pale kitambulisho kinapotumia QR Code, QR hiyo inaweza kutumika kuthibitisha uhalali wa kitambulisho na kuonyesha taarifa zilizoidhinishwa kwa ajili ya uthibitishaji. Wakala haruhusiwi kutengeneza kitambulisho kingine kinachofanana na kitambulisho rasmi cha Vortex Stay bila ruhusa.

5. Majukumu ya Wakala

Kutegemea kazi aliyoidhinishwa kufanya, wakala anaweza kupewa jukumu la:

  • Kutambulisha huduma za Vortex Stay;
  • Kutoa maelezo sahihi kuhusu huduma;
  • Kusaidia hoteli, lodge au watoa huduma kuelewa namna mfumo unavyofanya kazi;
  • Kusaidia katika mchakato wa usajili pale anaporuhusiwa;
  • Kutangaza Vortex Stay kwa kufuata miongozo rasmi ya kampuni;
  • Kufikisha changamoto au malalamiko ya wateja kwa Vortex Stay;
  • Kufanya shughuli nyingine ambazo Vortex Stay itamuidhinisha rasmi.

Wakala hatakiwi kuahidi huduma, bei, malipo, zawadi, punguzo au masharti ambayo hayajaidhinishwa na Vortex Stay.

6. Fedha na Malipo

Wakala haruhusiwi kukusanya fedha kwa niaba ya Vortex Stay isipokuwa pale amepewa mamlaka rasmi ya kufanya hivyo. Iwapo Vortex Stay itaanzisha mfumo wa kamisheni, bonus au malipo ya wakala:

  • Viwango vitaainishwa na Vortex Stay;
  • Malipo yatafanyika kwa njia zilizoidhinishwa;
  • Vortex Stay inaweza kuthibitisha shughuli kabla ya kulipa kamisheni;
  • Shughuli bandia hazitastahili kamisheni;
  • Kodi au makato yoyote yanayotakiwa kisheria yanaweza kufanywa kwa mujibu wa sheria.

Mtoa Huduma aliyesajiliwa na wakala ambaye anazalisha mapato yanayostahili kugawanywa chini ya mfumo wa Vortex Stay, mgawanyo wa mapato husika utakuwa kama ifuatavyo:

  • Wakala — Asilimia Ishirini (20%); na
  • Vortex Stay — Asilimia Themanini (80%).

Mgawanyo huu utatumika kwa mapato yanayotokana na shughuli halali na zinazotambulika na mfumo wa Vortex Stay kama Qualifying Transactions zinazohusiana na mtoa huduma aliyesajiliwa.

Hakuna wakala anayeruhusiwa kumtoza mteja ada binafsi kwa kutumia jina la Vortex Stay bila ruhusa rasmi.

7. Udanganyifu Umepigwa Marufuku

Wakala haruhusiwi:

  • Kusajili watu hewa.
  • Kutengeneza akaunti bandia.
  • Kutumia namba ya simu ya mtu mwingine bila ruhusa.
  • Kutumia picha ya mtu mwingine.
  • Kujisajili mara nyingi kwa lengo la kupata faida.
  • Kubadilisha taarifa za wateja kwa udanganyifu.
  • Kutengeneza booking au transaction bandia.
  • Kutengeneza ushahidi wa malipo wa uongo.
  • Kughushi Agent ID.
  • Kujaribu kupata kamisheni kwa shughuli ambazo hazikutokea.
  • Kutumia taarifa za Vortex Stay kufanya biashara binafsi isiyoidhinishwa.
  • Kutoa taarifa za siri kwa washindani au watu wasioidhinishwa.

Ukiukwaji unaweza kusababisha akaunti kusimamishwa au kufutwa na hatua nyingine kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.

8. Ulinzi wa Taarifa za Wateja

Wakala anaweza kupata taarifa fulani za mteja au mtoa huduma kwa sababu ya kazi yake. Wakala anatakiwa:

  • Kutumia taarifa kwa kazi aliyokabidhiwa pekee;
  • Kutotoa taarifa kwa mtu mwingine bila mamlaka;
  • Kutotengeneza database binafsi kutoka kwenye taarifa za Vortex Stay;
  • Kutotumia namba za simu za wateja kwa matangazo binafsi;
  • Kutopiga picha au screenshot za taarifa bila sababu ya kikazi;
  • Kutotuma taarifa kupitia WhatsApp, Telegram, email au njia nyingine bila ruhusa pale taarifa hiyo ni ya siri;
  • Kuripoti mara moja ikiwa simu, kitambulisho au kifaa chenye taarifa za kampuni kimepotea.

Taarifa binafsi za wateja ni lazima ziheshimiwe wakati wote.

9. Matumizi ya Jina na Nembo ya Vortex Stay

Jina, nembo, rangi, picha, mabango, video na alama za biashara za Vortex Stay zitatumika kwa kufuata miongozo ya kampuni. Wakala haruhusiwi:

  • Kubadilisha logo bila ruhusa;
  • Kutengeneza website au ukurasa unaojifanya kuwa website rasmi;
  • Kufungua account ya social media kwa jina la Vortex Stay bila ruhusa;
  • Kuchapisha kadi, mabango au vifaa vingine vinavyoweza kupotosha umma;
  • Kujifanya mmiliki, director au mwakilishi mwenye mamlaka ambayo hajapewa.
10. Mwenendo wa Wakala

Wakala anatakiwa:

  • Kuwaheshimu wateja;
  • Kutumia lugha yenye heshima;
  • Kuepuka vitisho au usumbufu;
  • Kutotoa taarifa za uongo;
  • Kutobagua wateja;
  • Kutofanya vitendo vinavyoweza kuliharibia Vortex Stay jina;
  • Kutii sheria za Tanzania;
  • Kutunza siri za kampuni na za watumiaji.
11. Uhusiano kati ya Wakala na Vortex Stay

Kujisajili kuwa wakala hakumaanishi moja kwa moja kuwa mtu huyo ni mfanyakazi wa Vortex Stay. Isipokuwa pale ambapo kuna mkataba tofauti wa maandishi, wakala atafanya kazi kwa masharti ya mpango wa uwakala uliokubaliwa na Vortex Stay. Wakala hana mamlaka ya kuingia mikataba kwa niaba ya Vortex Stay isipokuwa amepewa mamlaka hayo kwa maandishi.

12. Kusimamishwa au Kufungwa kwa Akaunti

Vortex Stay inaweza kusimamisha au kufunga akaunti ya wakala endapo:

  • Taarifa alizotoa ni za uongo;
  • Anahusika na udanganyifu;
  • Anatumia vibaya taarifa za wateja;
  • Analeta madhara kwa kampuni au watumiaji;
  • Anatumia kitambulisho cha mtu mwingine;
  • Anakiuka masharti haya;
  • Anakiuka sheria;
  • Akaunti yake inahusishwa na shughuli zinazotishia usalama wa mfumo.

Katika mazingira yanayofaa, wakala anaweza kupewa nafasi ya kueleza upande wake kabla ya uamuzi wa mwisho.

13. Kuacha Kuwa Wakala

Wakala anaweza kuomba kuacha mpango wa uwakala. Kuacha kuwa wakala hakufuti wajibu wowote uliokuwepo kuhusu:

  • Taarifa za siri;
  • Madeni halali;
  • Uchunguzi wa udanganyifu;
  • Kurejesha mali ya kampuni;
  • Wajibu unaoendelea chini ya sheria.

Kitambulisho cha wakala kinaweza kufutwa au kuwekwa kuwa hakitumiki baada ya uhusiano kusitishwa.

SEHEMU B — SERA YA FARAGHA YA MAWAKALA

14. Taarifa Tunazoweza Kukusanya

Taarifa za utambulisho: Majina kamili; Picha; Vortex ID/Agent ID; Taarifa nyingine za uthibitishaji pale zinapohitajika.

Taarifa za mawasiliano: Namba ya simu; Taarifa zinazohusiana na uthibitishaji wa OTP.

Taarifa za eneo: Mkoa; Wilaya; Tarafa; Eneo la kazi pale inapohitajika.

Taarifa za matumizi ya mfumo: Tarehe ya kujisajili; Tarehe na muda wa kuingia kwenye mfumo; Mabadiliko yaliyofanywa kwenye akaunti; Historia ya shughuli za wakala; Taarifa za kifaa na usalama; Audit logs zinazohitajika kwa usalama na uchunguzi.

15. Sababu za Kukusanya Taarifa

Taarifa zako zinaweza kutumika kwa: kusajili ombi lako la kuwa wakala; kuthibitisha namba yako ya simu; kuthibitisha utambulisho wako; kutengeneza Agent ID/Vortex ID; kupitia na kuidhinisha ombi lako; kusimamia akaunti yako; kuwasiliana nawe kuhusu kazi za uwakala; kuzuia udanganyifu; kulinda watumiaji na mfumo; kutekeleza malipo au kamisheni pale zinapohusika; kutatua malalamiko; kutekeleza masharti ya uwakala; kutimiza wajibu wa kisheria; kufanya ukaguzi wa usalama na audit.

Taarifa zako hazitatumika kwa madhumuni yasiyoendana na sababu ya kukusanywa bila msingi unaofaa wa kisheria.

16. Msingi wa Kuchakata Taarifa

Vortex Stay itachakata taarifa binafsi kwa kuzingatia sheria zinazotumika, ikiwa ni pamoja na pale ambapo: umetoa ridhaa inayohitajika; uchakataji unahitajika ili kutekeleza mchakato wa usajili au uhusiano wa uwakala; kuna wajibu unaotokana na sheria; uchakataji unahitajika kwa usalama, kuzuia udanganyifu au kulinda haki halali za kampuni au watumiaji, pale sheria inaporuhusu.

Pale uchakataji unapotegemea ridhaa, unaweza kuomba kuiondoa kwa mujibu wa sheria. Kuondoa ridhaa hakufanyi uchakataji uliokuwa halali kabla ya kuondolewa kwake kuwa batili.

17. Kushirikisha Taarifa na Wengine

Vortex Stay haitauza taarifa binafsi za mawakala. Taarifa zinaweza kushirikishwa kwa kiwango kinachohitajika na: watoa huduma za SMS/OTP; watoa huduma za hosting au cloud; watoa huduma za malipo pale inapohitajika; watoa huduma za usalama na teknolojia; wakaguzi au washauri wa kitaalamu; mamlaka za Serikali pale sheria inapohitaji; vyombo vya sheria pale kuna msingi halali wa kufanya hivyo.

Watoa huduma wanaopewa taarifa wanatarajiwa kutumia taarifa kwa madhumuni yaliyoidhinishwa na kwa kuzingatia mahitaji yanayotumika ya ulinzi wa taarifa.

18. Picha ya Wakala

Picha inayotolewa wakati wa usajili inaweza kutumika kwa: uthibitishaji wa utambulisho; kutengeneza kitambulisho; kuonyesha taarifa za Agent ID; kuzuia matumizi ya kitambulisho na mtu mwingine; uchunguzi wa udanganyifu. Picha haitakiwi kutumiwa kwa matangazo ya biashara bila msingi unaofaa au ruhusa inayohitajika.

19. Usalama wa Taarifa

Vortex Stay itachukua hatua zinazofaa za kiufundi na kiutawala kulinda taarifa dhidi ya: kupotea; kuibiwa; kubadilishwa bila ruhusa; kutumiwa vibaya; kufikiwa na mtu asiyeidhinishwa; kufutwa kimakosa; kuvuja kwa taarifa. Hatua hizo zinaweza kujumuisha udhibiti wa access, authentication, audit logs, encryption inapofaa, backups na ufuatiliaji wa usalama.

Wajibu huu utafanyika pia kwa Wakala kwa kuchukua hatua za msingi za kulinda akaunti yake, neno lake la siri (password), OTP na Agent ID.

20. OTP na Usalama wa Akaunti

OTP ni siri. Wakala hatakiwi: kutoa OTP kwa mtu mwingine; kutuma screenshot ya OTP; kumpa mtu mwingine ruhusa ya kutumia akaunti yake; kuingiza OTP kwenye website isiyo rasmi ya Vortex Stay. Vortex Stay haitakiwi kumuomba wakala kutoa OTP yake kwa njia isiyo salama kwa madhumuni ya kawaida ya support.

21. Muda wa Kuhifadhi Taarifa

Taarifa zitahifadhiwa kwa muda unaohitajika kutekeleza madhumuni yaliyokusudiwa, kutimiza wajibu wa kisheria, kutatua migogoro, kuzuia udanganyifu na kutekeleza masharti ya kampuni. Baada ya taarifa kutohitajika tena, zinaweza: kufutwa; kuharibiwa kwa usalama; kufanywa zisitambulike. Baadhi ya kumbukumbu zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu zaidi pale sheria au madai halali yanapohitaji.

22. Haki za Wakala Kuhusu Taarifa Zake

Kwa mujibu wa sheria zinazotumika, wakala anaweza kuwa na haki ya: kujulishwa taarifa zinazokusanywa na sababu zake; kuomba kuona taarifa zake; kuomba taarifa zisizo sahihi zirekebishwe; kuomba kufutwa kwa taarifa katika mazingira yanayoruhusiwa; kuomba uchakataji uzuiwe katika mazingira yanayoruhusiwa; kupinga aina fulani za uchakataji; kuomba kuhamisha taarifa pale sheria inaporuhusu; kuondoa ridhaa pale uchakataji unategemea ridhaa; kuomba ufafanuzi kuhusu maamuzi fulani ya kiotomatiki; kuwasilisha malalamiko kuhusu matumizi ya taarifa zake. Baadhi ya haki zinaweza kuwa na mipaka kulingana na wajibu wa kisheria wa Vortex Stay.

23. Kufuta Akaunti

Ombi la kufuta akaunti halimaanishi kwamba taarifa zote zitafutwa mara moja. Vortex Stay inaweza kuendelea kuhifadhi baadhi ya taarifa ikiwa zinahitajika: kutimiza wajibu wa sheria; kuzuia udanganyifu; kutatua mgogoro; kutekeleza mkataba; kuhifadhi kumbukumbu zinazotakiwa kisheria.

24. Uhamishaji wa Taarifa Nje ya Tanzania

Iwapo taarifa zitahifadhiwa au kuchakatwa nje ya Tanzania, Vortex Stay itazingatia masharti yanayotumika ya sheria kuhusu uhamishaji wa taarifa binafsi nje ya nchi na kuchukua hatua zinazohitajika kulinda taarifa hizo.

25. Taarifa za Watoto

Mpango wa uwakala unakusudiwa kwa watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi. Mtu aliye chini ya miaka 18 hatakiwi kujisajili kama wakala kupitia mfumo huu. Ikiwa Vortex Stay itagundua kuwa akaunti imesajiliwa na mtu aliye chini ya umri unaotambulika (miaka 18), inaweza kusimamisha akaunti hiyo na kuchukua hatua zinazotakiwa kuhusu taarifa husika kwa mujibu wa sheria.

26. Cookies na Taarifa za Kiufundi

Website inaweza kutumia cookies au teknolojia zinazofanana kwa madhumuni ya: kuwezesha login/session; kulinda akaunti; kuzuia matumizi mabaya; kuhifadhi preference zinazohitajika; kuboresha utendaji wa website. Cookies zisizo za lazima zitatumika kwa kuzingatia masharti yanayotumika kuhusu taarifa binafsi na ridhaa.

27. Tukio la Kuvuja kwa Taarifa

Endapo kutatokea tukio la usalama linalohusisha taarifa binafsi, Vortex Stay itafanya uchunguzi na kuchukua hatua zinazofaa za kurekebisha tatizo. Pale sheria inapohitaji, taarifa kuhusu tukio zinaweza kutolewa kwa mamlaka husika na/au watu walioathirika.

28. Malalamiko

Wakala anapaswa kwanza kuwasilisha suala linalohusu taarifa binafsi kupitia njia rasmi za mawasiliano za Vortex Stay. Haki hii haizuii mtu kutumia utaratibu mwingine wa malalamiko unaopatikana chini ya sheria za Tanzania, ikiwemo kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka yenye dhamana ya ulinzi wa taarifa binafsi. Malalamiko hayo yanaweza kuwasilishwa kupitia mfumo au barua pepe, na Vortex Stay itayapokea na kuyafanyia kazi. Ikiwa hakutokea utatuzi wa changamoto hiyo, wakala anaweza kutumia njia nyingine ya kisheria.

29. Mabadiliko ya Masharti

Vortex Stay inaweza kuboresha masharti haya kutokana na: mabadiliko ya huduma; mabadiliko ya mfumo; mabadiliko ya sheria; mahitaji ya usalama; mabadiliko ya mpango wa mawakala. Mabadiliko muhimu yatawasilishwa kwa njia inayofaa kabla au wakati yanapoanza kutumika. Toleo la sasa la masharti litapatikana kupitia mfumo rasmi wa Vortex Stay.

Endapo kutakuwa na mabadiliko ya kamisheni, hayataponguza au kuathiri kamisheni ambayo tayari imepatikana kutokana na muamala unaostahili (Qualifying Transaction) uliokamilika kabla ya kuanza kutumika kwa mabadiliko hayo.

30. Sheria Inayotumika

Masharti haya yataongozwa na sheria zinazotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogoro itashughulikiwa kwanza kwa njia ya mawasiliano na utatuzi wa ndani pale inapowezekana, bila kuondoa haki yoyote ambayo mhusika anayo chini ya sheria. Iwapo njia ya amani haitapatikana, upande husika unaweza kutumia mahakama yenye mamlaka kwa mujibu wa sheria ili kutatua mgogoro huo.

SEHEMU C — TAMKO LA WAKALA

Kwa kuweka alama kwenye kisanduku cha kukubali, nathibitisha kwamba:

  • Nina umri wa miaka 18 au zaidi;
  • Taarifa nilizowasilisha ni za kweli na sahihi;
  • Picha na namba ya simu niliyotumia ni yangu au nina mamlaka halali ya kuitumia;
  • Nimesoma na kuelewa Masharti ya Mawakala;
  • Nimesoma na kuelewa Sera ya Faragha;
  • Nakubali taarifa zangu zitumike kwa madhumuni ya usajili, uthibitishaji, utambulisho, usalama na usimamizi wa uwakala kwa mujibu wa sera hii;
  • Ninatambua kwamba kujisajili hakumaanishi nimeidhinishwa kuwa wakala mpaka Vortex Stay itakapokubali ombi langu;
  • Nitazingatia sheria, kanuni na maelekezo rasmi ya Vortex Stay.
MAWASILIANO

Kwa maswali kuhusu usajili, akaunti au taarifa binafsi:

Vortex Stay
Website: artificialintelligence.tz
Barua pepe: vortexrid@gmail.com
Simu: 255771559201
Anuani: Dar es Salaam